VITENDAWILI VYA KISWAHILI NA MAJIBU YAKE
**Vitendawili vya kiswahili na majibu yake**
**A\
1\. Adui lakini po pote uendako yuko nawe. Inzi\
2\. Afahamu kuchora lakini hajui achoracho. Konokono\
3\. Afuma hana mshale. Nungunungu\
4\. Ajenga ingawa hana mikono. Ndege\
5\. Ajifungua na kujifunika. Mwavuli\
6\. Akitokea watu wote humwona. Jua\
7\. Akitokea watu wote hunungunika na kuwa na huzuni. Ugonjwa\
8\. Akivaa nguo hapendezi, akiwa uchi apendeza. Mgomba\
9\. Alipita mtu ana bunda la mshale. Mkindu\
10\. Alipita mtu mwenye kibandiko cha nguo. Inzi\
11\. Aliwa, yuala; ala, aliwa. Papa\
12\. Amchukuapo hamrudishi. Kaburi\
13\. Amefunika kote kwa blanketi lake jeusi. Giza\
14\. Amefunua jicho jekundu. Jua\
15\. Ameingia shimoni akiwa uchi, akatoka amevaa nguo nzuri. Mbegu\
16\. Amejitwika mzigo mkubwa kuliko yeye mwenyewe. Konokono/Koa\
17\. Amekaa kimya na watoto wamemzunguka pande zote. Mgomba\
18\. Amekula ncha mbili. Wali\
19\. Amevaa joho kubwa kuliko yeye mwenyewe. Kaburi\
20\. Anakuangalia tu wala halali au kutembea. Picha\
21\. Anakula kila siku lakini hashibi na hatashiba. Mchanga\
22\. Anakula lakini hajashiba na hatashiba milele. Ardhi\
23\. Anakula lakini hashibi. Mauti\
24\. Anapendwa sana ingawaje ni mkali sana. Moto\
25\. Anatoka kutembea, anakuja nyumbani anamwambia mama, ‘Nieleke’. Kitanda\
26\. Ashona mikeka wala hailali. Maboga\
27\. Askari wangu wote wamevaa kofia upande. Majani\
28\. Askari wangu wote wamevaa mavazi meusi. Chunguchungu\
29\. Asubuhi atembea kwa miguu mine, adhuhuri kwa miwili. Fedha\
30\. Atapanya mbegu nyingi sana lakini hazioti. Mvua\
31\. Atolewapo nje hufa. Samaki\
B\
32\. Baba alinipa mfupa, nikautunza ukawa fahali. Muwa\
33\. Baba ameweka mkuki nje nikashindwa kuukwea, mdogo wangu akaukwea. Sisimizi\
34\. Babako akojoapo hunung’unika. Mawingu\
35\. Babu amefunga ushanga shingoni. Mtama/Nazi\
36\. Babu anakula ng’ombe, analea fupa linakuwa ng’ombe. Muwa\
37\. Babu hupiga kelele akojoapo. Mvua\
38\. Babu mkubwa ameangushwa na babu mdogo. Mti na shoka\
39\. Babu, nyanya, mjomba, mama, baba na watoto, mna safari ya wapi? Siafu\
40\. Bak bandika, bak bandua. Nyayo\
41\. Bawabu mmoja tu asiyeogopa chochote duniani. Mlango\
42\. Bibi kikongwe apepesa ufuta. Kope za macho\
43\. Bibi yake hutandikwa kila siku, lakini hatoroMoyoKinu cha kutwangia**
**C\
44\. Chakula kikuu cha mtoto. Usingizi\
45\. Cha ndani hakitoki nje, cha nje hakiingii ndani. Nyama na mfupa\
46\. Chang’aa chapendeza, lakini hakifikiwi. Jua\
47\. Chatembea na hakijapata kupumzika hata nukta moja. Mwezi/Jua\
48\. Cheupe chavunjika manjano yatokea. Yai\
49\. Chumba change kina ukuta niondoa na kuusimika nitakapo. Pazia\
50\. Chungu change cha udongo hakipasuki kikianguka. Mjusi/Panya\
51\. Chungu kikubwa sana chenye kifuniko kikubwa sana. Dunia na mbingu**
**D\
52\. Dada yangu akitoka kwao harudi kamwe. Jani likwanyukapo\
53\. Dada yangu kaoga nusu. Jiwe mtoni\
54\. Drrrrrh1 Ng’ambo. Daraja la buibui\
55\. Dume wangu amelilia machungani. Radi**
**F\
56\. Fahali wa ng’ombe na mbuzi wadogo machungani. Mwezi na nyota angani\
57\. Fika umwone umpendaye. Kioo\
58\. Fuko kajifukia, mkia kaacha nje. Kata mtungini\
59\. Funga mizigo twende Kongo. Mikia ya mbwa**
**H\
60\. Hachelewi wala hakosei safari zake. Jua\
61\. Haina miguu wala mikono, lakini, yabeba magogo. Maji\
62\. Hakihitaji maji, wala udongo, wala chakula; lakini chamea. Nywele\
63\. Hakionekani wala hakishikiki. Hewa\
64\. Hakisimami, na kikisimama msiba. Moyo\
65\. Hakuchi wala hakuchwi. Kula\
66\. Halemewi wala hachoki kubeba. Ardhi\
67\. Hamwogopi mtu yeyote. Njaa\
68\. Hana mizizi, nimemkata mara nyingi lakini haachi kukua. Ukucha\
69\. Haoni kinyaa. Mvua\
70\. Hapo nje panapita mtu mwenye miguu mirefu. Mvua\
71\. Hasemi, na akisema hatasahaulika. Kalamu\
72\. Hasimamishwi akiwa na ghadhabu. Upepo\
73\. Hata inyeshe namna gani haifiki humu. Kwapani\
74\. Hata jua likiwaka namna gani hakauki wala kupata joto. Pua ya mbwa\
75\. Hata Mzungu ameshindwa. Mauti\
76\. Hauchagui chifu wala jumbe. Utelezi\
77\. Hausimiki hausimami. Mkufu\
78\. Hawa wanaingia hawa wanatoka. Nyuki mzingani\
79\. Hesabu haihesabiki. Nyota\
80\. Huitumia kila siku lakini haiishi. Miguu\
81\. Huku kutamu, huku kutamu, katikati uchungu. Jua\
82\. Huku unasikia ‘pa’ Huku unasikia ‘pa! Mkia wa kondoo\
83\. Hula lakini hashibi. Sindano\
84\. Hulala tulalapo, huamka tuamkapo. Jua\
85\. Humu mwetu tuko wanne tu, ukimwona wa tano mwue. Matendegu ya kitanda\
86\. Huna macho lakini wakamata wanyama. Ndoana\
87\. Hupanda mtini na mwenye kichaa wake. Kivuli\
88\. Hutembea watatu. Mafiga\
89\. Hutoka upesi sana lakini hasalimu. Kuku\
90\. Huwafanya watu wote walie. Moshi\
91\. Huwezi kukalia alipokalia msichana wangu mweusi. Chungu jikoni\
92\. Huzikwa mmoja, hufufuka mmoja, huzeeka wengi. Mbegu na matunda**
**I\
93\. Inaonekana mara mbili katika dakika moja na mara moja tu katika mwaka. Herufi “K”\
94\. Ini la ng’ombe huliwa hata na walioko mbali. Kifo**
**J\
95\. Jembe la Wangoni haliishi. Miguu/Nyayo\
96\. Je, unaweza, kukua ukampita mzee wako? Nywele kichwani\
97\. Jiwe litoalo maji. Macho**
**K\
98\. Kaburi la mfalme lina milango miwili. Kata ya kuchukulia Maji kichwani\
99\. Kaka yangu anapanda darini na fimbo nyuma. Paka na mkia wake\
100\. Kama kingekuwa mkuki, ungekuta kimekwisha kuua wote. Kizingiti cha mlango\
101\. Kama unapenda, mbona usile? Ulimi\
102\. Kanipa ngozi nikapikia, kanipa nyama nikala, kanipa mchuzi nikanywa, kanipa mfupa nikautumia. Nazi\
103\. Kapanda mti pamoja na uchawi wake. Tumbaku inaponuswa puani\
104\. Kidimbwi kimezungukwa na majani. Macho\
105\. Kikioza hutumiwa, kikiwa kichungu hakitumiwa. Maziwa\
106\. Kila linapofika kwetu hutanguliza makelele. Mvua\
107\. Kila mtu atapitia malango huo. Kifo\
108\. Kila mtu hata mfalme huheshimu akipita. Mlango\
109\. Kila siku hupita njia hiyo hiyo bali arudipo hatumwoni. Jua\
110\. Kileee! Hiki hapa. Kivuli\
111\. Kilimsimamisha chifu njiani. Chawa\
112\. Kina mikono na uso lakini hakina uhai. Saa\
113\. Kinaniita lakini sikioni. Mwangwi\
114\. Kisima cha Bimpai kina nyoka muwai, ndiye fisadi wa maji. Taa ya utambi\
115\. Kisima kidogo kimejaa changarawe. Kinywa na meno\
116\. Kitendawili change ukikitambua nitakupa hirizi. Mimba\
117\. Kiti cha dhahabu hakikaliwi na watu. Moto\
118\. Kiti cha Sulatni hukaliwa na mwenyewe. Kuku aatamiapo mayai\
119\. Kiti nyikani. Uyoga\
120\. Kitu changu asubuhi chatembea kwa miguu mine, saa sita kwa miguu miwili, jioni kwa miguu mitatu. Maisha ya binadamu\
121\. Kiwanja kizuri lakini hakifai kuweka mguu. Kipara\
122\. Kombe ya Sultani Ii wazi. Kisima\
123\. Kondoo wangu amezaa kwa paja. Mhindi\
124\. Kondoo wangu mnene kachafua njia nzima. Konokono\
125\. Kondoo za mtoto zamaliza mavuno. Jiwe la kusagia\
126\. Kufanya kwa ridhaa mojamoja. Kusuka mkeka\
127\. Kuku wangu aliangua mayai jana, lakini si kuku wala ndege. Nyoka au samaki\
128\. Kuku wangu amezalia miibani. Nanasi au chungwa\
129\. Kuku wetu hutagia mayai mikiani. Matunda\
130\. Kuna mlima mmoja usio pandika. Nafasi kati mdomo na pua\
131\. Kuna mtu mwenye tumbo kubwa aliyesimama nje. Ghala\
132\. Kuna ziwa kubwa ambalo limekauka na limebakiza mizizi. Chongo\
133\. Kunguru akilia hulilia mirambo. Mtoto akililia maziwa\
134\. Kwenye msitu mkubwa Napata mti mmoja tu, lakini kwenye msitu mdogo naweza kupata miwili. Watoto wa ng’ombe na mbuzi\
135\. Kwetu mishale na kwenu mishale. Mikia ya panya\
136\. Kwetu twalala tumesimama. Nguzo za nyumba**
**L\
137\. La mgambo limelia wakatoka weusi tu. Chunguchungu\
138\. Likienda hulia, likirudi halilii. Debe aka buyu\
139\. Likitoka halirudi. Neno\
140\. Liwali amekonda lakini hana mgaga. Sindano**
**M\
141\. Mama ametengeneza chakula lakini hakula. Chungu cha kupikia\
142\. Mbona kinakumeza lakini hakikuli? Nyumba\
143\. Mbona mwakunjiana ngumi bila kupigana? Mafiga\
144\. Mbona mwasimama na mikuki, mwapigana na nani? Katani\
145\. Mchana ‘ti’ usiku ‘ti’. Mlango\
146\. Mdogo lakini humaliza gogo. Mchwa\
147\. Mfalme amesimika mkuki wake hapa name nikausimika wangu kando yake, baadaye\
hatukuitambulisha tena. Kohozi\
148\. Mfalme hushuka kwa kelele. Mvua\
149\. Mfalme katikati lakini watumishi pembeni. Moto na mafiga\
150\. Mfalme wetu hupendwa sana, lakini wakati wa kumwona lazima umtoe nguo zote kwanza. Hindi\
151\. Mhuni wa ulimwengu. Inzi\
152\. Mkanda mrefu wafka mpaka pwani. Njia\
153\. Mke wangu mfupi, lakini huvaa nguo nyingi. Hindi\
154\. Mlango wa nyumba yangu uko juu. Shimo la mchwa\
155\. Mlima mkubwa wapandwa kuanzia juu. Sima/Ugali\
156\. Mlimani sipandi. Maji\
157\. Mlima umezuia kutazama kwa mjomba. Kisogo\
158\. Mlima wa kupanda kwa mikono. Mlima\
159\. Mlima wa kwetu hupandwa na mfalme. Nafasi kati ya mdomo na pua ya ngombe\
160\. Mlima wa mwenyewe hupandwa na mwenyewe. Buibui na utando wake\
161\. Mpini mmoja tu lakini majembe hayahesabiki. Mkungu wa ndizi\
162\. Msitu ambao haulii hondohondo. Mimba\
163\. Mti mkubwa, lakini una matawi mawili tu. Kichwa na masikio\
164\. Mti mnyanya mti kerekeche mti ah mti ah!. Ngoma na upatu\
165\. Mti wangu una matawi kumi na mawili na kila tawi lina majani kadiri ya thelathini. Mwaka\
166\. Mtoto asemea pangoni. Ulimi mdomoni\
167\. Mtu mdogo mwenye miguu mirefu ambaye aweza kutembea dunia nzima kwa dakika tano. Mawazo\
168\. Mvua hema na jua hema. Kobe\
169\. Mvua kidogo ng’ombe kaoga kichwa. Jiwe\
170\. Mwadhani naenda lakini siendi. Jua\
171\. Mwalimu analala na mwanafunzi wanamsomea. Kinyesi na inzi\
172\. Mwanamke mfupi hupiga kelele njiani. Kunguru\
173\. Mwanamke mfupi hutengeneza pombe nzuri. Nyuki\
174\. Mwanang’ang’a hulia mwituni. Shoka\
175\. Mwepesi, lakini aweza kuvunja nyumba za mji wote. Tufani\
176\. Mwezi wangu umepasuka. Kweme\
177\. Mzee Kombe akitoa machozi wote hufurahi. Mvua\
178\. Mzee Kombe akilia watu hufurahi. Mvua\
179\. Mzizi wa miti hutokea mbali. Siafu\
180\. Mzungu yuko ndani na ndevu ziko nje. Hindi**
**N\
181\. Naitumia ngazi hiyo kwa kupandia na kushukia. Mwiba\
182\. Nakikimbilia lakini sikikuti. Njia\
183\. Nakupa lakini mbona huachi kudai. Tumbo\
184\. Nakwenda msituni na mdogo wangu, lakini yeye namwacha huko.\
185\. Nameza lakini sishibi. Mate\
186\. Namkimbiza lakini simkuti. Kivuli\
187\. Namlalia lakini halii. Kitanda\
188\. Namwomba atangulie lakini hukataa kabisa. Kigino\
189\. Nanywa supu na nyama naitupa. Muwa\
190\. Napigwa na mvua na nyumba ipo. Matunda ya pua/Kwapa\
191\. Natembea juu ya miiba lakini hainichomi. Miiba\
192\. Natembea juu ya miiba lakini sichomwi. Ulimi\
193\. Natembea na wenzangu lakini tukifika kwenye nyumba mimi hukaa mlangoni. Mbwa\
194\. Natengeneza mafuta lakini nimepauka sana. Mzinga was nyuki kwa nje\
195\. Natengeneza mbono lakini alama hazionekani. Mzinga wa nyuki\
196\. Ndege wengi baharini. Nyota\
197\. Ndugu wawili wafanana sana, lakini hawatembeleani. Macho\
198\. Ngoja nikumbuke. Boga changa\
199\. Ng’ombe wa baba watelemka mtoni. Mawe mtoni\
200\. Ng’ombe wa babu huchezea miambani. Mijusi\
201\. Ng’ombe za babu zikienda machungani hulia, zikirudi hazilii. Vbuyu\
202\. Ng’ombe za babu zinalala na mkia nje.Viazi vitamu udongoni\
203\. Ng’ombe wamechanganyika nikakosa wa kwangu. Pesa/Nyayo\
204\. Ng’ombe wangu ni weupe kwatoni. Katani\
205\. Ng’ombe wangu wote hunywa maji isipokuwa mmoja. Fimbo ya kuchunga\
206\. Ngozi ndani nyama juu. Firigisi\
207\. Nguo ivaliwayo kila siku isiyoingiwa na chawa. Nyusi\
208\. Nikicheka kinacheka, nikinuna kinanuna. Kioo\
209\. Nikienda arudi, nikirudi aenda. Kivuli majini\
210\. Niiita ‘baba’ huitika ‘baba’. Mwangwi\
211\. Nikija kwenye ndege wananifukuza, na nikienda kwenye wanyama hawanitaki. Popo\
212\. Nikimpiga huyu huyu alia. Utomvu wa papai\
213\. Nikimpiga mambusu. Puliza kidole wakati unapojikwaa\
214\. Nikimwita hunijibu nani. Mwangwi\
215\. Nikipewa chakula nala bali natema. Shoka\
216\. Nikitembea walio wafu huniamkia na walio hai hukaa kimya. Majani makavu na mabichi\
217\. Nikitembea yuko, nikikimbia yuko, nikiingia ndani hayupo. Kivuli\
218\. Ni kitu gani ambacho kutoa ni kuongeza? Shimo\
219\. Nikitupa mshale wangu mchana huenda mbali sana, lakini niutupapo usiku hauendi mbali. Jicho\
220\. Nikiwaambia ondokeni hukataa, lakini mjomba akitokea wote hukimbia. Umande na jua\
221\. Nilijenga nyumba yangu nikaiacha bila kuiezeka majani; lakini niliporudi nilikuta imekwisha ezekwa majani. Mahindi machanga\
222\. Nilijenga nyumba yangu yenye mlango mmoja. Jani la mgomba la nchani\
223\. Nilimkata alafu nikamridhia. Kupanda mbegu\
224\. Nilimtuma askari vitani akaniletea kondoo mweusi. Fuko\
225\. Nilipandia majanini nikashukia majanini. Mwiba\
226\. Nilipigwa na tonge la ugali la moto nilipopita msituni. Manyigu\
227\. Nilipitisha mkono wangu chini la ardhi, nikamshika beberu mkubwa sana. Kiazi kikuu\
228\. Nilipoangalia kwenye magereza ya Wazungu, nikaona wameketi juu ya mabati. Pelele\
229\. Nilipofika msituni nilikuta chungu cha pure kinachemka. Mzinga wa nyuki\
230\. Nilipoingia Rumi, alitoka mtu na wake kumi; kila mke na tundu kumi, kila tundu na kuku\
kumi; kila kuku na mayai kumi. Mayai, kuku, tundu, wake, kumi kumi kumi. Wangapi\
walikwenda Rumi? Hakuna\
231\. Nilipo, juu kuna miiba na chini vivyo hivyo; lakini sichomwi. Ulimi kinywani\
232\. Nilipokuwa mchanga nilikuwa na kijikia lakini sasa sinacho. Chura\
233\. Nilitembea na mwezangu naye hupita vichakani. Kivuli\
234\. Nimechoma fimbo yangu pakabaki pa kushikia tu. Njia\
235\. Nimefyeka mitende yote kiungani isipokuwa minazi miwili tu. Masikio\
236\. Nimejenga nyumba babu akaihamia kabla mimi sijahamia. Mjusi\
237\. Nimekata mti, akaja samba mwekundu akaukalia. Utomvu\
238\. Nimekata mti bara ukaangusha matawi pwani. Nzige\
239\. Nimekwenda na rafiki yangu kwa jirani, yeye akafika kabla yangu. Sauti ya nziga\
240\. Nimemtahiri binti wangu akatoa damu mchana kutwa. Kivuli\
241\. Nimempeleka kondoo wangu akatoa damu mchana kutwa. Mgomba\
242\. Nimemtuma mtu kumwamkua mtu, yeye amekuja, Yule aliyetumwa hajaja. Kuangua tunda Ana nazi\
243\. Nimemwacha mzee kikongwe mtoni anangojea mgeni kulaki. Mtego\
244\. Nimempandikiza mti wangu ukapeleka matawi ng’ambo ya mto. Kivuli\
245\. Nimesimama mbali nyikani lakini naonekani. Moto\
246\. Nimetembea kitambo, kukumbuka sikufunga nyumba. Dirisha Ana ufa\
247\. Nimetoka kutembea kutembea, nikashika ng’ombe mkia. Kata\
248\. Nimetupa mshale angani wala sitambui utateremsha ndege wa namna gani. Mimba\
249\. Nimeweka ndizi yangu, asubuhi siioni. Nyota\
250\. Nimezaliwa na mguu mmoja. Uyoga\
251\. Nimezungukwa na adui wengi, lakini siumizwi. Ulimi na meno\
252\. Nina kijiti change, nizidivyo kukikata ndivyo kizidivyo kuwa kirefu. Maisha\
253\. Nina kitu changu kitumiwacho na wengine kuliko mimi. Jina\
254\. Nina kitu kizuri sana nyumbani, lakini siwezi kukichukua. Dada\
255\. Nina kitu nipendacho ambacho hata baba, mama, dada, kaka hata na mgeni nimpendaye sana siwezi kumwazima. Mke\
256\. Nina mwezi ndani ya bakuli. Maziwa\
257\. Nina ng’ombe wangu nisipomshika mkia hali majani. Jembe\
258\. Nina nyumba yangu imezungukwa na mifupa. Mdomo\
259\. Nina pango langu lilojaa mawe. Kinywa\
260\. Nina watoto wangu hamsini na wote nimewavisha visibau vyeupe. Kunguru\
261\. Nina watoto watatu, mmoja akitoka kazi haifanyiki. Mafiga\
262\. Nina badilika umbo langu baada ya kila muda mfupi. Kivuli\
263\. Ninachimba mizizi ya mti usio na mizizi. Jiwe\
264\. Ninacho, nakitumia, lakini kila nikitumiapo, sikiharibu ila nakipa rangi. Maji na mkojo\
265\. Ninakula vitu vyote vinono lakini sikui wala sinenepi. Chungu cha kupikia\
266\. Ninakwenda naye na kurudi naye. Kivuli\
267\. Ninao mlima ambao una msitu kileleleni tu. Kichwa\
268\. Nitokeapo kila mmoja asema namtazama yeye tu. Jua au mwezi\
269\. Njia yapitwa siku zote lakini haina alama. Njia ya jua au mwezi\
270\. Njoo hapa nije hapo. Kiraka\
271\. Nne nne mpaka pwani. Matendegu\
272\. Nusu mfu nusu hai. Sungura alalapo\
273\. Nyama ndogo imewashibisha wengi wala isiishe. Kinoo\
274\. Nyama ya Reale haijai kikombe. Mkufu\
275\. Nyanya yako ana huruma kukubeba ulalapo. Kitanda\
276\. Nyumba yangu ina makuti tele, lakini mvua ikinyesha huvuja. Mwembe\
277\. Nyumba yangu ina milango mingi. Kichuguu\
278\. Nyumba yangu ina nguzo moja. Uyoga\
279\. Nyumba yangu kubwa, haina mlango. Yai\
280\. Nyumba yangu kubwa, haina taa. Kaburi\
281\. Nyumba yangu kubwa hutembelewa mgongoni. Konokono**
**O\
282\. Oh! Mwanamke aliyevunja chungu mshangao wake\
283\. Ondoka nikae. Maji ya mfereji**
**P\
284\. Paa alipenga hata pua ikapasuka. Mbarika\
285\. Palikuwepo watu watatu wakivuka mto. Mmoja alivuka pasipo kukanyaga maji wala kuyaona; wa pili aliyaona maji lakini alivuka bila kuyakanyaga; wa tatu aliyaona na kuyakanyaga alipovuka.\
Ni nani hawa? Was kwanza in Mtoto tumboni mwa mamake, was pili ni Mtoto aliyebebwa mgongoni, was tatu ni mama mwenyewe\
286\. Panda ngazi polepole. Sima ya ugali\
287\. Para hata Maka. Utelezi\
288\. Pete ya mfalme ina tundu katikati. Kata ya kuchukulia mizigo\
289\. Poopoo mbili zavuka mto. Macho\
290\. Po pote niendako anifuata. Kivuli**
**R\
291\. Rafiki yangu ana mguu mmoja. Uyoga\
292\. Reli yangu hutandika ardhini. Siafu\
293\. Ruka Riba. Maiti**
**S\
294\. Shamba langu kubwa lakini mavuno hayajazi kiganja. Nywele kichwani\
295\. Shamba langu miti mitano tu. Mkono wa vidole\
296\. Shangazi yangu ni mrefu sana lakini hafikii tumbo la kondoo. Njia\
297\. Sijui aendako wala atokako. Upepo\
298\. Sijui afanyavyo. Nyoka apandavyo mtini\
299\. Sina dada wala kaka, lakini baba wa huyu jamaa ni mtoto wa babangu. Ni nani huyo? Mtoto wangu\
300\. Subiri kidogo! Miiba\
301\. Sultani alipiga mbiu watu waje kufanya kazi yake lakini wakashindwa. Maji**
**T\
302\. Taa ya bure. Jua au mwezi\
303\. Taa ya Mwarabu inapepea. Kilemba\
304\. Tajiri aniweka mfukoni na maskini anitupa. Makamasi\
305\. Tandika kitanga tule kunazi. Nyota\
306\. Tangu kuzaliwa kwake sijamwona asimame wala kukimbia. Mkufu\
307\. Tatarata mpaka ng’ambo ya mto. Utando wa baibui\
308\. Tatu tatu mpaka pwani. Mafiga\
309\. Tega nikutegue. Mwiba\
310\. Teke teke huzaa gumugumu, na gumugumu huzaa teke teke. Mahindi ama yai\
311\. Tengeneza kiwanja kikubwa kabila Fulani lije kupigania. Mbono\
312\. Tonge la ugali lanifikisha pwani. Jicho\
313\. Tukate kwa visu ambacho hakitakatika. Maji\
314\. Tulikaribishwa mahali na mdogo wangu, yeye akaanza kushiba kabla yangu. Kucha\
315\. Tuliua ng’ombe na babu, kila ajaye hukata. Kinoo\
316\. Tuliua ng’ombe wawili ngozi ni sawasawa. Mbingu na nchi\
317\. Tumvike mwanamke huyu nguo. Kuezeka nyumba\
318\. Tunajengajenga matiti juu. Mapapai\
319\. Twamsikia lakini hatumwoni. Sauti**
**U\
320\. Ukimcheka atakucheka, ukimwomba atakuomba. Mwangwi\
321\. Ukimwita kwa nguvu hasikii, lakini ukimwita polepole husikia. Fisi\
322\. Ukimwona anakuona. Jua\
323\. Ukitaka kufahamu ana mbio, mwonyeshe moto. Kinyonga\
324\. Ukitembea ulimwengu wote utakosa nyayo. Mwamba\
325\. Ukiukata haukatiki, ukiushika haushikiki. Moshi\
326\. Ukiwa mbali waweza kumwona Fulani umatini. Tundu LA sindano\
327\. Ukoo wa liwali hauna haya. Wanyama\
328\. Ule usile mamoja. Kifo\
329\. Umempiga sungura akatoa unga. Funds LA mbuyu\
330\. Unatembea naye wote umjiao atakuona. Bakora\
331\. Upande wote umjiao atakuona. Kinyonga\
332\. Ushuru wa njia wKujikwaa Kujikwaa\
333\. Utahesabu mchana na usiku na hutamaliza kuhesabu. Nywele**
**V\
334\. Viti kumi nyumbani, tisa vyakalika lakini kimoja hakikaliki. Moto**
**W\
335\. Wake wa mjomba kimo kimoja. Vipande vya kweme\
336\. Wako karibu lakini hawasalimiani. Nyumba ama kuta zinazoelekeana\
337\. Wanakuja mmoja mmoja na kujiunga kuwa kitu kimoja. Matone ya mvua\
338\. Wanameza watu jua linapokuchwa. Nyumba\
339\. Wanamwua nyoka. Watu wanaotwanga\
340\. Wanangu wawili hugombana mchana, usiku hupatana. Mlango\
341\. Wanao wakati wao wa kuringa, nao ni weupe kama barafu. Nyota\
342\. Wanapanda mlima kwa makoti mazuri meusi na meupe. Vipepeo\
343\. Wanastarehe darini. Panya\
344\. Wanatembea lakini hawatembelewi. Macho\
345\. Watoto wa mtu mmoja hulala chini kila mwaka. Maboga\
346\. Watoto wangu wana vilemba, asio kilemba si mwanangu. Fuu\
347\. Watoto wangu wote nimewavika kofia nyekundu. Jogoo\
348\. Watoto wangu wote wamebeba vifurushi. Vitovu\
349\. Watu ishirini walipanda juu ya mti, wawili wakaona chungwa, watano wakalichuma, kumi wakalimenya, wote wakaridhirika mtu mmoja alile. Je, ni watu gani hao? Waliopanda ni vidole vya miguu na mikono, walioona ni macho mawili, waliochuma ni vidole vitano vya mikono, waliomenya ni vidole vya mikono yote miwili, na aliyelila ni mdomo\
350\. Watu waliokaa na kuvaa kofia nyekundu. Kuku, katani au mahindi\
351\. Watu wamehama askari wekundu wakazidi nyikani. Viroboto\
352\. Watu wawili hupendana sana; kati ya mchana hufuatana ingawa mmoja ni dhaifu. Usiku mdhaifu\
haonekani tena. Kivuli\
353\. Watu wote ketini tumfinye mchawi. Kula ugali\
354\. Wewe kipofu unaenda wapi huko juu? Mkweme**
**Y\
355\. Yaenda mbali lakini haiondoki ilipo. Njia**
**Z\
356\. Zilitazamana na mpaka sasa hazijakutana. Kingo za mto\
357\. Ziwa dogo linarusha mchanga. Chungu jikoni\
358\. Ziwa kubwa, lakini naogelea ukingoni tu. Moto**